Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Afisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar - AGCZ

Bendera ya Taifa
Kuhusu Afisi

Historia ya Afisi ya Mwanasheria Mkuu

Safari ya kihistoria ya Afisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar tangu kuanzishwa kwake hadi sasa.

Jengo la zamani la Afisi ya Mwanasheria Mkuu
Jengo la zamani la Afisi ya Mwanasheria Mkuu hadi mwaka 2013

Kabla ya Mapinduzi ya 1964

Afisi ya Mwanasheria Mkuu ni miongoni mwa taasisi kongwe zilizoanzishwa Zanzibar katika kipindi cha utawala wa kikoloni mnamo mwaka 1913–1914. Kazi yake kuu ilikuwa kutoa ushauri wa kisheria kwa Serikali na kusimamia masuala ya kisheria kwa niaba ya Serikali.

Mwaka 1926 Mwanasheria Mkuu alikuwa miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria na Utawala, akiendelea kushiriki katika masuala ya kisheria hadi kipindi cha Mapinduzi ya mwaka 1964.

Jengo la sasa la Afisi ya Mwanasheria Mkuu
Jengo la sasa la Afisi ya Mwanasheria Mkuu kuanzia mwaka 2014

Baada ya Mapinduzi ya 1964

Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Afisi ya Mwanasheria Mkuu iliendelea kutekeleza majukumu ya kisheria kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Nafasi ya Mwanasheria Mkuu ilitambuliwa rasmi ndani ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 chini ya kifungu cha 55(1).

Kwa sasa, kazi na majukumu ya Afisi yameongezeka kwa mujibu wa Sheria ya Afisi ya Mwanasheria Mkuu (Utekelezaji wa Majukumu) Nam. 6 ya mwaka 2013, sambamba na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kiutawala.

Historia Kamili ya Afisi

Faili la PDF lina maelezo ya kina kuhusu historia, mabadiliko na maendeleo ya Afisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar.

Pakua PDF