Mhe. Dkt. Mwinyi T. Haji
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar (2020–Sasa)
Historia
Amehudumu katika nyadhifa mbalimbali za kitaaluma, kiutawala na kisheria. Tangu mwaka 2020 hadi sasa, amekuwa akihudumu kama Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Kabla ya hapo, aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje mwaka 2020, Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kuanzia mwaka 2018 hadi 2020, Mkurugenzi wa Masomo ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Zanzibar kuanzia mwaka 2013 hadi 2018, Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Zanzibar kuanzia mwaka 2012 hadi 2017, Msaidizi wa Mhadhiri kuanzia mwaka 2007 hadi 2012, pamoja na Mshauri wa Kisheria katika Wizara ya Maji na Ardhi kuanzia mwaka 2005 hadi 2007.