Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi Talib Haji, amesema Afisi yake imewapandisha madaraja Mawakili wa Serikali Hamsini na Nane (58) kutoka wizara na taasisi mbali kuwawezesha mbali, ili kutekeleza vyema majukumu yao.
Mhe. Mwanasheria Mkuu alieleza hayo wakati akitoa ufafanuzi wa maswali mbali mbali yaliyoulizwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wa kuchangia Bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Sheria katika Mkutano wa Tatu wa Baraza la Kumi na Moja huko katika Ukumbi wa Baraza Chukwani, Zanzibar.
Dkt. Mwinyi aliahidi kuwa Afisi yake kuwapandisha madaraja maafisa sheria wengine kulingana na mahitaji ili kuimarisha uwezo wa kitaaluma na maarifa katika majukumu yao ikiwemo ya kuitetea Serikali.
Alifahamisha kuwa kupitia kasi ya maendeleo yanayofanywa na Serikali na kazi ngumu zinazoendelea kufanywa, upo umuhimu wa kuwaongezea hadhi na majukumu Maafisa Sheria pamoja na Mawakili wa Serikali ambao wapo katika wizara na taasisi mbali mbali za umma.
“Hatuwezi kumpandisha daraja kila Wakili ama Afisa Sheria, katika kufanya hivyo ni lazima tuzingatie uwezo wake na mahitaji ya Serikali”, alisema Mwanasheria Mkuu. Dkt. Serikali Mwinyi kupitia alisema Afisi ya Mwanasheria Mkuu itaendelea kuwajengea uwezo Maafisa sheria na Mawakili wake kwa kuwapa mafunzo ndani na nje ya nchi, sambamba na kuimarisha maslahi yao.
Alisema hatua hiyo husaidia kuimarisha uwezo wa Mawakili katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo kuisimamia vyema Serikali katika kutatua kesi mbali mbali za madai, ushauri na usimamizi wa mkkataba inayofikishwa kwenye taasisi waliopo.
Dkt. Mwinyi alifafanua kuwa tangu kuunganishwa kwa Tume ya Kurekebisha Sheria na Afisi ya Mwanasheria Mkuu, Sheria tisa zimefanyiwa mapitio, ambapo Sheria mbili zimeshawasilishwa katika sekta husika, huku Sheria mbili zikiwa katika hatua ya kupokea maoni kutoka kwa wadau.
"Nadharia ya Serikali kuijumuisha Tume ya Kurekebisha Sheria katika Afisi ya Mwanasheria Mkuu, ni kuijengea uwezo zaidi na madhumuni yake ni kuonesha namna Tume hiyo inavyoendelea kutekeleza majukumu yake chini ya Afisi ya Mwanasheria Mkuu”, alifafanua.
Awali Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi akiwemo Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mhe. Nadir Yussuf Al-wardy waliipongeza Afisi ya Mwanasheria Mkuu kwa namna inavyotoa ushauri wake wa kitaalamu juu ya Mikataba ya Serikali ambayo inaletwa katika Afisi hiyo.
Walisema licha ya Serikali ya Awamu ya Nane kuwa na ongezeko la mikataba mingi, Afisi hiyo inaendelea kujitahidi kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wakati na kuirejesha mikataba hiyo kwa taasisi.
Habari
18 May 2026
51 views
Mwanasheria Mkuu: Tutaendelea Kupandisha Madaraja Mawakili
Muhtasari:
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi Talib Haji, amesema Afisi yake imewapandisha madaraja Mawakili wa Serikali Hamsini na Nane (58) kutoka wizara na taasisi mbali kuwawezesha mbali, ili kutekeleza vyema majukumu yao.